MWANA WA KUKU
Yu wapi huyu Mabula, banda halina meneja
Tena kenda na msala, kuendeleza harija
Anakufanyia hila, kukusakia wateja
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Ukichinjwa akukula, wa kwanza kutaka paja
Ukiuzwa kwa Mabala, wakwanza fedha kufuja
Leo karuka Unguja, mebaki huna faraja
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Ukiuzwa kwa Mabala, wakwanza fedha kufuja
Leo karuka Unguja, mebaki huna faraja
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Siende kwa majalala, pasi ruhusa ya mja
Kurukaruka holela, na uache mara moja
Nakuonya halahala !,haya nasema kwa tija
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Kurukaruka holela, na uache mara moja
Nakuonya halahala !,haya nasema kwa tija
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Kipanga ananyemela, humwoni anavyokuja
Jifanye kwenda pahala, eti umepata haja
Utabakia salala !,takavyofanywa kioja
Mwana wa kuku lala,kipanga yuwaja
Jifanye kwenda pahala, eti umepata haja
Utabakia salala !,takavyofanywa kioja
Mwana wa kuku lala,kipanga yuwaja
Jambo hili mjadala, kama ulivyo mkaja
Karibuni mawakala, neno kwa mshika leja
Sipendezwi na madhila, natoa ya kwangu hoja
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
Karibuni mawakala, neno kwa mshika leja
Sipendezwi na madhila, natoa ya kwangu hoja
Mwana wa kuku lala, kipanga yuwaja
©2014 Na Innocent Zephania.
No comments:
Post a Comment