Monday, 9 January 2017

MIKIA MTATOKAJE















Golini yupo batezi,, kama wa ufaransa
Mpira hautelezi,, akidaka umenasa
Sabu yake didazi,, kwenye benchi ananesa
SIMBA MTATOKAJE??
Kuna juma abduli,, huyu ni beki kitasa
Kiiza amjua vizuli,, shaidi wetu mkwasa
Anajua kukabili,, nyavu hamtogusa
SIMBA MTATOKAJE??
Osca mwana joshua,, atatulia kushoto
anakaba na kuzuia,, wapinzani tumbo joto
Simba wataumia,, tuwaweke kitimoto
SIMBA MTATOKAJE???
kuna baba canavaro,, huyu ndo mwenye nyumba
Huyu hajui usharo,, hapa kazi anavimba
Simba wa mvomero,, leo anapata mimba
SIMBA MTATOKAJE???
Unamjua twite,, ananguvu sijaona
acha mpira upite,, faulu karusha kona
anajua putepute,, mbona mikia itakoma
SIMBA MTATOKAJE??
sijamtaja kamusoko,, atayesimama kati
alilete sokomoko,, mshikane mashati
Kisha apige moko,, mikia mpira kati
SIMBA MTATOKAJE???
kuna tambwe bin tambwe,, nadhani mnamjua
Magoli ayafunge,, kwa shoto na kulia
Kama ngumi mkinge,, maana mmezoea
SIMBA MTATOKAJE???
kuna donald ngoma,, huruma nawaonea
Mwaka huu mtaisoma,, namba ya kikuria
Magoli yake mapema,, kabla jua kuchwea
SIMBA MTATOKAJE???

No comments:

Post a Comment