RAFIKI MNAFIKI
Liapa hutoki, kwa raga na dhiki,
Miye kasadiki, nawe kaafiki,
Kumbe baramaki, haja yako keki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Miye kasadiki, nawe kaafiki,
Kumbe baramaki, haja yako keki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Mola kabariki, kapata riziki,
Wali kwa samaki, asali ya nyuki,
Lipokuja dhiki,kaniona taki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Wali kwa samaki, asali ya nyuki,
Lipokuja dhiki,kaniona taki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Kawa sidiriki, kesha mishikaki,
Ukaanza chuki, kija hunilaki,
Kajaza hamaki, hupiki hudeki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Ukaanza chuki, kija hunilaki,
Kajaza hamaki, hupiki hudeki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Kapungua maki, uki kawa siki,
Kaisha ashiki, kabania haki,
Ukawa shabaki, wa pembe za chaki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Kaisha ashiki, kabania haki,
Ukawa shabaki, wa pembe za chaki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Kaja taharuki, kashindwa shaliki,
Hali kuhakiki, iwe tutaliki,
Lekuwa maliki, kawa "kitu hiki",
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Hali kuhakiki, iwe tutaliki,
Lekuwa maliki, kawa "kitu hiki",
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Nimeshinda cheki, zawadi lukuki,
Gari pikipiki, shida sikumbuki,
Usirudi Njoki, na penzilo feki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
Gari pikipiki, shida sikumbuki,
Usirudi Njoki, na penzilo feki,
Machoni rafiki, moyoni nafiki.
No comments:
Post a Comment