KISWAHILI
Huyu hapa Mmachinga, napitia vibambani,
Siuzi nguo na kanga, kwa wateja mitaani,
Nawajuvya kwa kulonga, tajiri na masikini,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.

Mbele lugha inasonga, malipyoto mashakani,
Vibwebwe tumejifunga, kuendeleza hi' fani,
Wapingao watachonga, waletao ushindani,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Vibwebwe tumejifunga, kuendeleza hi' fani,
Wapingao watachonga, waletao ushindani,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Naionea fahari, lugha hino unganishi,
Imelijaza bohari, kwa mazuri maandishi,
wanopenda wana kheri, nawavisha tarabushi,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Imelijaza bohari, kwa mazuri maandishi,
wanopenda wana kheri, nawavisha tarabushi,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Hino ni yetu wadau, mbona sasa malumbano,
Litakwama letu dau, kwa yetu mafarakano,
Ruwaza tusisahau, kisa eti mapambano,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Litakwama letu dau, kwa yetu mafarakano,
Ruwaza tusisahau, kisa eti mapambano,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Twapigana kisa ngeli, pia eti tafusiri,
Naona twacheza geli, kulumbania fasiri,
kukikuza kiswahili,tuyaache machachari,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Naona twacheza geli, kulumbania fasiri,
kukikuza kiswahili,tuyaache machachari,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Acheni nifike hapo, japo mengi sijasema,
Kumbukeni KAZI IPO, na yatupasa kusoma,
Sisikilize michapo, bali soma taaluma,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
Kumbukeni KAZI IPO, na yatupasa kusoma,
Sisikilize michapo, bali soma taaluma,
Lugha ipo yenye hadhi, jina lake Kiswahili.
No comments:
Post a Comment